Busara za baba

Mambo siku zote huwa mepesi kwa wenye ufahamu, lakini upumbavu wa mpumbavu ni zaidi ya udanganyifu . yaani namaanisha kuwa rafiki wa mpumbavu / mjinga daima am
tegemea maumivu . Bado naamini kuwa sio wote wenye mbio washindao vitani,wala sio wore walio hodari washindao vitani, wala sio wote wenye elimu wapatao Mali , wala sio wote wenye uwezo watapewa upendeleo ila naamini katika mambo matatu katika hii dunia kwanza bahati pili mida na mwisho uwezo / ustadi vitu hivyo usivitegemee sana katika maisha yako amino uwezo  unao na pia wapo wengi wenye uwezo kama wako amino unaweza wa kutengeneza mambo ndani ya kichwa chako na yakakusaidia kuwa katika nafasi Fulani , lazima ujue kuwa dunia haina mida wa kutosha hivyo tumia muda sawasawa kila upatapo nafasi usiseme muda hupo ukiamini muda hupo hautafanikisha mambo mengi. Na pia kuna uwezo usifikirie kuwa hauna uwezo,uwezo unao ila haujautumia na kuendeleza ujuzi wako.


Lazima ujenge maisha yako kichwani ndipo uyaweke katika maisha ya kawaida yaani namaanisha usiwe na maisha ya mtizamo Bali uwe na mawazo imara na fikra yakinifu na kutamani mafanikio , lazima ujenge bifu na umasikini , lazima ujenge ukatili wa kupigania mafanikio bila kukata tamaa , lazima ukubali kuhumiza kichwa , ubongo na mwili katika kutafuta mafanikio bila kuchoka , na mwisho lazima ujenge moyo wa wa matendo sambamba na fikra zenye kuona kuona mbali na zenye matendo ndipo utakapoweza kuona pambazuko la mafanikio na matumaini katika maisha yako.

Lazima uingie katika vita Kali ya kupambana na uwoga inakupasa ujue adui mkubwa wa mafanikio ni uwoga , uwoga wa kujaribu ,uwoga wa kutenda ,uwoga wa kuuliza ,uwoga wowote ule unarudisha nyuma ubunifu wa Nazi ,ubunifu wa maendeleo pamoja na ubunifu wa mafanikio. AMEN

Comments

Popular posts from this blog

Elimu ni ufunguo wa maisha

Maendeleo yanapatikanaje?

Unataka kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali