Ushauri kwa vijana

Kama tunavojua kuwa vijana ndio nguvu kazi ya jamii hivyo hatuna budi kufanya juu chini ili kuonyesha nguvu kazi yenywe lakini vijana wengi wamesahau hili na kuishia kuketi kwenye vijiwe wakidiscus mambo yasiyo na msingi ktk maisha badala ya kushirikiana na familia zetu katika kuinua uchumi tumegeuka na kuwa wadidimizaji wa uchumi katika familia zetu tunashindana kununua Jordan,supreme,Gucci kwa kutumia fedha ya familia badala ya kukesha kuitafuta iyo hela tunakesha tukiitumia uchumi was familia unashuka na sisi tunazidi kuudidimiza tumegeuka kuwa soko adimu la bidhaa za kielectronic tunakesha ktk mitandao Mara Instagram Mara Facebook Mara Twitter Mara IMO Mara Snapchat atufanyi mambo ya maendeleo zaidi ya kuchat mambo yasiyo na faida na mambo tunayoyajua sio mbaya kuitumia hizi social network Bali tunazitumia vipi kwa maendeleo yetu au ?

Tunakesha vijiweni tukisema amna kazi Mara Magufuli kabana tunakesha tukijadili watu badala ya kukesha tukitumia fursa zinazotuzunguka vijana wengi sana elimu ya kutosha lakini wanasema amna ajira wanakesha mitaani wakitegemea ajira ziwafuate wakiwa wameeka vyeti kabatini atutaki kujiajiri kwa kutumia fursa zinazotuzunguka Bali tunahofia elimu yako unaogopa ukifanya kazi ya chini utaonekana wa hali ya chini wakati unaelimu ya kutosha tunasahau kuwa Bakhressa akuzaliwa tajiri Bali alizitumia changamoto kama fursa ata Dangote akuzaliwa tajiri Leo hii wasio na elimu wanafkiri awawezi kufanikiwa awataki kutumia vipaji vyao kama fursa wanasahau mahali Diamond Platinum alipofikia sio elimu Bali alitumia kipaji chake kama fursa na kipaji chake kinamfanya ategemewe badala la kutegemea atutaki kutumia fursa za kawaida zinazotuzunguka tunasubiri ajira miaka miwili unakula ugali wa baba yako unavaa kwake unalala kwake unakunywa kwake unakuwa tu mzigo badala ya kutumia fursa zilizopo.

Bila kugeuka,vijana tutalipoteza taifa letu kwa maana linapoelekea saivi linaonekana linapotea.


   Ndio maana nasema ni bora kufa ukiwa na fikra zilizo hai kuliko kuishi
           na fikra zilizo kufa 





Kwa ushauri zaidi 0743106296 WhatsApp only

Comments

Popular posts from this blog

Elimu ni ufunguo wa maisha

Maendeleo yanapatikanaje?

Unataka kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali