Maendeleo yanapatikanaje?
Maendeleo ni kaziwww.mawazoimara@gmail.com
Maendeleo ni jitihada
Maendeleo ni kujitoa kutafuta mafanikio
Maendeleo ni utashi na utayari wa kutumikakiakili na kimwili.
Maendeleo ni hasira ya kupambana na upungufu.
Maendeleo ni fikra zenye kuona mbali na kutamani mafanikio.
Maendeleo ni juhudi na nidhamu.
Maendeleo ni wewe.
Lazima vijana tuelewe kuwa maendeleo hayatokani na kubweteka na umahiri wa kulalamika hapana maendeleo hayako hivyo wala maendeleo hayatokoni na maombi na miujiza kwamba IPO siku MUNGU akakuwezesha kulala masikini na kukuamsha tajiri mwenyewe maendeleo makubwa hapana.
Maendeleo ni kazi na kuchangamkia fursa zilizopo ndani na nje ya uwezo wetu , maendeleo ni jitihada na juhudi zako.
Kila kukicha fursa mpya zinagundulika na zipo zinatuzunguka zinasubiri tuzifanyie kazi. Vijana ni lazima tuchangamkie fursa hizo badala ya kukaa na kubweteka , kulalamika na kushauriana ujinga.
Inawezekanaje kila sina ya simu tunaijua , kila aina ya wasanii tunawajua ,kila aina ya starehe tunafanya ,kila aina ya simu tunajua ,kila aina ya mitandao ya kijamii tunaijua na kuitumia alafu tunashindwaje kutumia fursa lukuki zinanazotuzunguka kila siku na kila kukicha.
Pasipo kujitambua vijana wengi tumegeuka kuwa walalamikaji ,tumegeuka kuwa soko adimu la bidhaa za elekroniki ,tumegeuka kuwa waporaji wa uchumi wa familia ili kuendeleza kununua vitu visivyokuwa na tija katika maisha yetu kama simu za bei ya juu , nguo za thamani ili uonekame na jamii kwamba unaenda na wakati. Lakini si kweli na tunazidi kuendeleza starehe badala ya uzalishaji.
Hatuzalishi chochote isipokuwa kulalamika na kusubiri bahati nasibu zitukute tukiwa tunapiga stori vijiweni , tukiwa tunaperuzi kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram,WhatsApp au Skype na mingine tuijuayo bila kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
Uchumi wa familia unashuka na tunazidi kuushusha na kuudidimiza.
Vijana ni lazima tushinde vishawishi hivyo na vipingamizi hivyo kwa kuongeza maarifa , ubunifu , kujitambu , kutumia fursa zilizopo , kufanya kazi kwa bidii na kujituma na kwa umakini.
Iko hivyi vijana tuanze na kujitambua kisha tufanye kazi kwa kujituma na kwa ubunifu , tujenge uthubutu wa kuwekeza na kujaribu fursa mpya , tujenge nidhamu na umakini mkubwa wa hali ya juu wa kutumia tulichonacho na kubwa zaidi tuukomboe muda kwa mambo ya msingi.
Ndipo tutakapopata na kuona pambazuko jema la maendeleo kwa mtu mmoja mmoja , familia pamoja na jamii kwa ujumla.
Usisite kutembelea ukurasa huu kupata somo la ( TUNAWEZA KUFANIKIWA )
ili uweze kujijenga zaidi kuhusu mafanikio yako.www.mawazoimara

Comments