Mambo ya kuzingatia ili kukuza biashara

Wengi tulio na biashara tunahitaji kuzikuza na kuweza kuzifanikisha ila tunasahau kuwa ili kukuza na kufanikisha biashara yako kuna mambo muhimu ya kuzingatia mambo nayo ndio nataka Leo niyaelezee kuanzia moja hadi lingine shuka na Mimi ili tuweze kwenda sawa.

Ila kabla ya kuzungumzia ayo mambo matatu ya muhimu nilazima tujue haya mengine ambayo pia ni muhimu katika biashara yoyote hile ambayo nayo yatasaidie kupanua wigo wa biashara yako katika jamii kwanza kabisa katika biashara yako ni lazima uwe na heshima kwa Wateja wako...................

Usiwe MTU wa kugombana gomba na wateja wako mteja wako unatakiwa umfanye mfalme aimaanishi umnyenyekee kupita kiasi Bali mhudumie mteja wako vizuri adi na yeye aone amani ndipo atakapo jisikia amani ili kesho arudi tena hivyo utafanya biashara yako ionekane imara usiwe MTU wa kushusha watu thamani yaani unaona mteja huyu ni wa thamani kuliko huyu hii itapelekea kupoteza Wateja na biashara yako ikadorora ukaanza kumtafuta mchawi nani kumbe wewe ndo mganga unae jichawia pia katika biashara kuwa na imani na umtegemee aliyekuweka duniani kwani matendo yote bila imani ni kazi bure.
         
                           3E'S
 Maana yake ni herufi tatu za E hizi herufi ni za kuzingatia sana katika biashara yako herufi hizi zina maana zifuatazo:-
  1. ECONOMY

  2. EFFICIENCY

  3. EFFECTIVENESS



                       ECONOMY
Kama tunavojua uchumi tumekuwa tukisikia uchumi wa nchi Mara umeshuka Mara umepanda  wapo wanaoelewa pia wapo wasiojua maana yake ni nini uchumi ni Yale mambo tunayoyafanya iwe ni uzalishaji usambazaji au biashara inayotuletea kipato huo tunasema ndio uchumi hivyo basi wewe kama wewe unatakiwa ulinde uchumi wako kwa Bali na Mali ili usipungue Bali uongezeke haina budi kuhakikisha unaongoza mambo yako ipasavyo ujaribu kutokuweka gap namaanisha unatakiwa kuziheshimu kazi zako ili uonemafanikio lakini uchumi hautaweza kusimama imara pasipo kuwepo na jambo hili ambalo ni la muhimu sana katika maisha yako ya kibiashara

            EFFICIENCY

Kwanza kabisa unatakiwa ujue maana ya efficiency ,efficiency maana yake ni uufanisi hapa ni kuangalia uwezo wako na idea yako katika iyo biashara unayokwenda kuifanya ili uifanikishe lazima utafute au use na ufanisi mkubwa katika kufanya iyo biashara yako hii itakusaidia kiendesha biashara yako kwa ufanisi mkubwa ambao utawazidi wale wanao Fanya biashara kama yako ufanisi wako ni muhimu kwani ukiwa MTU wakutegemea kuangalia mwenzako anafanya nini na wewe ndo ufanye utakuwa unapoteza mwelekeo katika kufanikisha biashara yako jambo la mwisho la kuangalia katika maisha yako ya kibiashara ni kama biashara yako inafaida nayo ni:-

                    EFFECTIVENESS

Effectiveness maana yake ni tija apa ni mafanikio na faida unayopata kutokana na biashara zako lazima uwe na kiasi lazima utumie faida kwa kuheshimu biashara yako usitumie zaidi ya mile unachopata lazima utumie faida tuu katika mambo yako mengine ambayo ayapo katika biashara yako hii itakusaidia sana katika kuzidi kuikuza biashara yako ukizingatia hayo lazima utaona mafanikio katika maisha yako hivyo ni bora na ni vizuri kuzingatia vitu hivyo vitatu economy,efficiency na effectiveness mafanikio yatafuata maisha yako.

Nashukuru kwa mda wako uliotumia kusoma pia nakukumbusha kumkumbuka muumba wako kwani bila yeye tutapatashida sana kumbuka kuwa aliyekupa pumzi ya kupumua ni yeye na uweke akilini kuwa unayoyatenda MUNGU anakuona na kwa mfano akija Leo itakuwaje hivyo nawashauri binadamu wenzangu tujue kuwa tunayoyafanya aliye juu anatuona na kama akija atatukutaje hivyo tunapokosea tusisahau kumuomba msamaha kwa maana anasamehe AMEN.

Usikose kutembelea ukurasa huu siku ya kesho kwa mengi yatakayo kuwa na faida katika maisha yako nakushukuru kwa mda wako uliotumia kusoma ukurasa huu na nakuombea siku njema.

Comments

Popular posts from this blog

Elimu ni ufunguo wa maisha

Maendeleo yanapatikanaje?

Unataka kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali